Box Office 020 7401 9919

booktickets browseplays

follow us

  • YouTube Channel

The Merry Wives of Windsor | Bitter Pill & Theatre Company Kenya

nini, basi dunia yangu chaza

'Why, then the world's mine oyster' 

Akifikiria kwamba Bi Ford na Bi Page wana hisia za kimapenzi kwake, mweheshimiwa John Falstaff anaamua kuwatongoza wote wawili kwa uzuri wao na haswa kwa sababu ya mali za mabwana zao. Hekima yao ikashinda ujanja wake uliopitwa na wakati, wanawake wakayageuza mambo na kumuaibisha Falstaff mara kathaa, kwanza kwa kumtumbukiza ndani ya kikapu cha dobi kilichojaa nguo nyevunyevu zenye uvundo mkali. Hiki ni kichekesho cha Shakespeare kinachohusu uchumba ambao haukufaulu, kilichopewa sauti ya Kiafrika. Bitter Pill inawaletea tafsiri yao ya ‘Wanawake wa Heri wa Windsor’ kutoka Nairobi hadi Uingereza. Mchezo huu umejawa na vichekesho na unasheherekea jinsi wanawake wa Kiafrika wanavyojitegemea kwa kutumia ujanja na werevu wao haswa wale wanaoishi mashambani. Kabla ya kusafiri kaskazini kuingiliana na ucheshi wa lugha ya Swahili, mchezo huu uliigizwa mwanzo kwenye Jumuiko la Sanaa la Kimataifa mjini Harare, Zimbabwe.

 

Tarehe, saa, kiingilio


Jumatano, Tarehe 25, Aprili, saa 14:30
Alhamisi, Tarehe 26, Aprili, saa 19:30